Askofu anayepinga ndoa za jinsia moja asusia mkutano Uingereza

Image caption Askofu anayepinga ndoa za jinsia moja asusia mkutano Uingereza

Mmoja wa viongozi wakuu wa kanisa la kianglikana nchini Uganda, amesema kuwa atahudhuria mkutano unaokuja wa viongozi wa kanisa la Anglikana ambao utafanyika mwezi Oktoba nchini Uingereza, kwa sababu hakubaliani na wale ambao wameanza kukubali ndoa za jinsia moja.

Askofu mkuu wa Uganda Stanley Ntagali aliiambia BBC kuwa hakuwa tayari kukutana na wale wanaokubaliana na kile alichokitaja kuwa ndoa zisizoambatana na mafunzo ya Biblia.

Alisema amefanya uamuzi huo baada ya kuomba ushauri kutoka kwa viongozi wengine nchini Uganda.

Wakatai wa mkutano uliopita wa viongozi wa dunia uliofanyika Januari mwaka 2016, Askofu Stanley Ntagali aliamua kuondoka mapema na kutisha kutorudi tena ikiwa hali hiyo haitarekebishwa.

Tangu wakati huo makanisa ya kianglikana ya Scotland na Canada yameunga mkono ndoa za jinsia moja.

Mada zinazohusiana