Walinzi wa Trump kuifanyia majaribio ndege ya ulinzi

President Trump driving a golf buggy Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Walinzi wa Trump kuifanyia majaribio ndege ya ulinzi

Walinzi wa rais wa Marekani Donald Trump wana mipango ya kufanyia majaribio ndege ya ulinzi isiyo na rubani wakati Trump atazuru klabu yake ya gofu huko New Jersey baadaye mwezi huu.

Ndege ndogo itafanyiwa majaribio na walinzi wa rais katika uwanja wa Trump National Golf Club huko Bedminster

Trump anatarajiwa kufanya ziara ndefu katika klabu hiyo.

Walinzi wa rais wanasema kuwa watazifanyia majaribio ndege kadhaa zisizo na rubani kwa masuala ya ulinzi.

Wakati wa shughuli hii ndege hiyo itaruka umbali wa kati ya futi 300 na 400 au mita 91 na 121 angani.

Ndege hiyo ina kamera pande tofauti na walinzi wa Trumo wanasema watajulisha watu katika klabu kuwa ndege hiyo itakuwa ikihudumu eneo hilo.

Walinzi hao wanasema kuwa makao ya kibinafsi yanaweza kunaswa na kamera za ndege hiyo.

Picha na video ambazo zinatarekodiwa na ndege hiyo zitafutwa baada ya siku 30.

Mada zinazohusiana