Mwanamume aliyeingizwa kwenye jeneza Afrika Kusini atoa ushahidi Mahakamani

Theo Jackson na Willem Oosthuizen Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Theo Jackson na Willem Oosthuizen

Mwanamume mmoja mweusi ambaye anadaiwa kulazimishwa kuingia ndani ya jeneza na wanaume wawili wazungu ambao walitisha kumchoma akiwa hai ametoa ushahidi mbele ya mahakama nchini Afrika Kusini.

Victor Mlotshwa alingua kilio kwenye mahakama kuu ya Middleburg wakati alikumbuka kisa hicho cha mwezi Agosti mwaka uliopita.

Mahakama ilicheza video ya kisa hicho ambapo bwana Mlotshwa anaweza kusokika akilia na kuomba washambuliaji kumsamehe.

Haki miliki ya picha youtube
Image caption Kisa hicho kilizua ghadhabu kubwa nchini Afrika Kusini.

Anadai kuwa wakulima Theo Jackson na Willem Oosthuizen walimfunga kwa nyaya wakampiga na kutishia kumpiga risasi.

Washukiwa hao wawili wanakana hilo wakidai kuwa walimpata bwana Mlotswa akiiba nyaya.

Wanasema kuwa lengi lao lilikuwa ni la kumfunza adabu. Kisa hicho kilizua ghadhabu kubwa nchini Afrika Kusini.

Mada zinazohusiana