Oscar Pistorius apelekwa hospitali kufanyiwa ukaguzi

Oscar Pistorius Haki miliki ya picha AFP
Image caption Pistorius alikuwa mwanariadha aliyetambulika kimataifa kabla ya kuhukumiwa kwa mauaji ya mpenzi wake

Mwanariadha huyo wa zamani wa mashindano ya Olimpiki Oscar Pistorius amepelekwa hospitalini, maafisa wamethibitisha.

Pistorius alifungwa gerezani kwa miaka 6 mnamo 2016 kwa mauaji ya mpenzi wake, Reeva Steenkamp.

Taarifa rasmi imethibitisha kuwa Pistorius "leo asubuhi amepelekwa katika hospitali ya nje ya gereza kufanyiwa ukaguzi wa kiafya".

Taarifa kuhusu hali inayomsibu Pistorius haikufichuliwa, lakini anatarajiwa kusalia hospitalini usiku kucha.

Msemamjiwa taasisi za nidhamu Afrika kusini ameliambia shirika la utangazaji nchini SABC kwamba kulazwa kwake hospitalini sio kwa "kitu kisicho cha kawaida" in Pistorius'.

Taasisi hiyo aidha imepuuzilia mbali taarifa kwamba Pistorius amelazwa hospitalini kutokana na "mamumivu ya kifua".

"Sifahamu taarifa hiyo au anachougua," msemaji mmoja ameliambia shirika la habari la Reuters.

Pistorius aliwahi kulazwa hospitalini mnamo Agosti mwaka 2016, baada ya kuteleza gerezani na kujeruhi viganja vyake vya mkono.

Mwanariadha huyo wa zamani alipata umaarufu wa haraka katika mashindano ya Olimpiki kwa walemavu, na kugonga vichwa vya habari kwa kuwa mwanariadha wa kwanza kushindana katika mashindano ya olimpiki - aliposhindana na wanariadha wasio walemavu na pia mashindano ya olimpiki kwa walemavu.

Lakini mnamo 2013 alimpiga risasi na kumuua Reeva Steenkamp nyumbani kwake, akidai alidhani na mhalifu aliyeivamia nyumba yake.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii