Jumba refu lachomeka Dubai

Jumba refu la Torch Tower huko Dubai likichomeka
Image caption Jumba refu la Torch Tower huko Dubai likichomeka

Moto mkubwa umelichoma mojawapo ya jumba refu duniani Torch Tower huko Dubai UAE kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka miwili.

Picha zilizowekwa katika mitandao ya kijamii zilionyesha moto huo ukisambaa hadi katika jumba hilo huku vifusi vilivyokuwa vikichomeka vikianguka.

Mamlaka baadaye ilisema kuwa wafanyikazi walifanikiwa kuwaondoa watu na wakafanikiwa kuudhibiti moto huo.

Haijulikani ni nini kilichosababisha moto huo katika mojawapo ya jumba refu dunaini.

Image caption Jumba refu la Torch Tower UAE

Hakuna majeraha yoyote yalioripotiwa kufikia sasa katika jumba hilo la Torch Tower ,kulingana na mamlaka ya Dubai iliotuma ujumbe katika Twitter.

Jumba hilo la Torch Tower liliharibiwa na moto mwengine 2015.