Rihanna awapatia wasichana wa Malawi baiskeli za kwenda shule

Rihana awapatia wasichana wa Malawi baiskeli za kwenda shule
Image caption Rihana awapatia wasichana wa Malawi baiskeli za kwenda shule

Rihanna anawapatia wasichana nchini Malawi baiskeli ili kuwasaidia kupata elimu.

Ni mojawapo wa ushirikiano kati ya Wakfu wa mwanamuziki huyo wa Clara Lionel Fountaion na kampuni moja ya baiskli kutoka China Ofo.

Kampeni hiyo kwa jina 1km Action itatoa ufadhili huo ili kuwasaidia mamia ya wasichana kuhudhuria shule za upili nchini malawi.

Wale watakaofuzu kupata ufadhili huo watapewa baiskeli ili kuhakikisha wanakwenda shule.

Kulinga na wakfu huo kuna takriban wanafunzi milioni 4.6 nchini malawi lakini ni asilimi nane pekee wanaokamilisha masomo yao ya shule za upili.

Sababu moja ya hali hiyo ni kutokana na ukosefu wa huduma ya uchukuzi.

''Nina furaha sana kuhusu ushirikiano wa wakfu wa Clara na Ofo kwa sababu utawasaidia wasichana wengi dunini kupata elimu bora'' ,alisema Rihanna, ''na pia kuwasaidia wasichana hao wa Malawi kwenda shule wakiwa salama, na kupunguza mwendo mrefu kutoka nyumbani kwenda shuleni.