Wafungwa Kenya wasubiri fursa ya kipekee ya kupiga kura

Wafungwa Kenya wasubiri fursa ya kipekee ya kupiga kura

Maelfu ya wafungwa kutoka magereza mbalimbali nchini Kenya kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya uchaguzi nchini watapata fursa ya kupiga kura.

Kwa sababu wafungwa wanatoka maeneo mbalimbali lakini wote wameandikishwa katika magereza yao, hawataruhusa kuwapigia kura viongozi wa mahali walipotoka na hivyo watampigia kura Rais pekee.

Wafungwa wengi na wanaharakati wamesifia hatua hiyo waliyoiita muhimu katika haki za wafungwa na demokrasia nchini Kenya.

Mwandishi wetu Sammy Awami ametuandalia taarifa ifuatayo.