MC Njagi: Mwanamuziki aliyevuna wanasiasa walipoteleza Kenya

MC Njagi: Mwanamuziki aliyevuna wanasiasa walipoteleza Kenya

Wakati mwanasiasa wa Kenya Wavinya Ndeti aliboronga methali ‘Yaliyopita si ndwele’ na kusema ‘Yaliyondwele sipite’ hakujua kwamba angepata umaarufu mtandaoni na kumpa msanii maneno ya kutunga wimbo ambao umempa umaarufu kote Kenya.

Wakati wengine walikuwa wakimbeza Wavinya kwenye mtandao wa Twitter kwa kutumia WavinyaChallenge, ‘MC Njagi’ alikuwa akitunga wimbo kwa kutumia methali hiyo, na sasa amekuwa kivutio cha wengi wakiwemo wanasiasa.

Video: Anthony Irungu