Korea Kaskazini kuwekewa vikwazo zaidi

Rais Kim Jong un wa Korea Kaskazini
Image caption Rais Kim Jong un wa Korea Kaskazini

Wanadiplomasia kwenye Umoja wa Mataifa mjini NewYork wanasema kuwa baraza ya ulinzi la Umoja wa Mataifa, leo litapigia kura azimio la kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini kutokana mpango wake wa zana za kinuklia.

Ripoti zinasema kuwa azimio lililoandaliwa na Marekani limeungwa mkono na Urusi na pia China.

Azimio hilo linajamuisha marufuku ya kuizuia Korea Kaskazini kuuza nje bidhaa kama mkaa wa mawe ambao huiletea Korea Kaskazini takriban dola bilioni moja kila mwaka.

Kura hiyo inapigwa wakati waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson, anaanza ziara ya Kusini mashariki mwa Asia ambapo anatarajiwa kutafuta uungwaji mkono kwa hatua kali dhidi ya Korea Kaskazni.