Ndege ya kijeshi ya Marekani yaanguka pwani ya Australia

Ndege ya wanamaji wa Marekani aina ya USS Ronald Regan Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndege ya wanamaji wa Marekani aina ya USS Ronald Regan

Operesheni ya uokoaji inafanyika baada ya ndege ya kijeshi ya Marekani kupotea katika pwani ya Australia.

Kisa hicho kilichoshirikisha ndege aina ya MV-22 Osprey inayomilikiwa na wanamaji wa Marekani inatoka eneo la Okinawa nchini Japan.

Kitengo cha wanamaji cha tatu kilisema kuwa ndege hiyo ilipaa kwa opresheni za kawaida kabla ya kuingia majini.

Makundi ya waokoaji yaliwanusuru watu 23 lakini maafisa wengine 3 hawajapatikana.

Vyombo vya habari vya Australia vimeripoti kwamba kisa hicho kilitokea wakati wa jaribio kutua katika meli ya kubeba ndege.

MV 22 Osprey inaweza kubeba watu 24 mbali na wafanyikazi 4.

Iko sawa na ndege ya kawaida lakini ina mbawa kama yale ya helikopta ambayo huisaidia kupaa wima.

Gazeti la la telegraph nchini Australia ilinikuu duru za kijeshi ambazo zinasema kuwa kisa hicho kilitokea wakati ndege hiyo ilipokuwa ikijaribu kutua katika meli ya kubeba ndege za kijeshi ya USS Ronald Reagan