Justin Gatlin amshinda Usain Bolt mbio za mita 100

Gatlin Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Justin Galtlin amshinda Usain Bolt mbio za mita 100

Justin Gatlin alizima matumaini ya Usain Bolt ya kustaafu kutoka riadha akiwa kileleni aliposhindwa wakati wa mbio za mita 100 kwenye mashindano ya IAAF mjini London.

Bolt alimaliza mbio hizo katika nafasi ya tatu na kushinda shaba huku Christian Coleman mwenye umri wa miaka 21 akichukua nafasi ya pili.

Gatlin mwenye umri wa miaka 35 ambaye alipigwa marufuku mara mbili alikimbia laini ya saba kwa muda wa sekunde 9.92.

Haki miliki ya picha .
Image caption Matokeo

Gatlin bingwa wa mita 100 mwaka 2004 na bingwa mara mbili mwaka 2005, alikuwa amekemewa na umati wakti wote kila mara kufuatia historia yake ya kupigwa marufu kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu za mwili.

Baada ya kugunduliwa mara ya pili mwaka 2006 aliponea kupigwa marufuku maishani alipokubali kushirikiana na mamlaka na kukubali marufuku ya miaka minane ambayo baadaye ilipunguzwa hadi miaka minne baada ya kukata rufaa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bolt (kushoto) na Coleman (kulia)

Hatua hiyo ilimruhusu kurejea tena mbioni.

Hata hivyo umati ulijibua kwa kumshangilia Usain Bolt wakati matokeo yalipotokewa hiyo jana.

Bolt mwenye umri wa miaka 30 hajawai kupoteza mbio za mita 100 katika ubingwa wa dunia.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bolt akimpongeza Gatlin

Mada zinazohusiana