Marekani yasitisha shughuli ya kutafuta wanajeshi waliotoweka baharini

Three MV-22 Osprey aircraft flying in formation above the Pacific Ocean off the coast of Sydney, Australia, on 29 June Haki miliki ya picha AFP
Image caption Marekani yasitisha shughuli ya kutafuta wanajeshi waliotoweka baharini

Maafisa nchini Marekani wamesitisha oparesheni ya kutafua wanajeshi watatu ambao wametoweka baada ya ndege yao kuanguka nje ya pwani wa Australia.

Kisa hicho cha siku ya Jumamosi kilihusu ndege ya MV-22 Osprey inayomilikiwa na kikosi kilicho na kambi huko Okinawa Japan.

Kikosi kinachoendesha shughuli ya kuwatafuta kinasema sasa kimeanzisha oparesheni yaa kutafuta inayoweza kudumu miezi kadhaa.

Familia za wanajeshi hao watatu zimejuliswa. Makundi yaliwaokoa watu 23.

Kilichosababisha kuanguka kwa ndegr hiyo bado kinafanyiwa uchunguzi.

Kulikuwa na watu 26 ndani ya ndege hiyo.

Huwezi kusikiliza tena
MV-22 Osprey

Gazeti la Daily Telegraph lilinukuu taarifa za kijeshi zikisema kuwa ndege hiyo imekuwa ikijaribu kutua kwenye meli ya kivita ya USS Ronald Reagan.

Vikosi vya Marekani vimekuwa vikihudumu eneo kama sehemu ya mazoezi ya pamoja yanayojuliana kama Talisman Sabre yanayowajumuisha wanajeshi 30,000 kutoka nchi zote mbili.