China yaitaka Korea Kaskazini kusitisha majaribio ya makombora

People"s Republic of China Foreign Minister Wang Yi gestures as he is escorted by Zhao Jianhua, Chinese ambassador to the Philippines, upon arrival at the international airport of Pasay to attend the 50th ASEAN Foreign Ministers meeting, metro Manila, Philippines August 5, 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wang Yi anasema alimshauri Ri Yong-ho kuheshimu maazimio ya Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano wao uliofanyika nchini Ufilipino.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa China amemuambia mwenzake wa Korea Kaskazini kuwa Korea Kaskazini itahitaji kusitisha majaribio ya makombora baada ya vikwazo vipya vilivyowekwa na baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa.

Wang Yi anasema alimshauri Ri Yong-ho kuheshimu maazimio ya Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano wao uliofanyika nchini Ufilipino.

Hata hivyo hakusema vile bwana Ri alijibu.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Korea Kaskazini Ri Yong-ho

Siku ya Jumamosi baraza la usalama la Umoja wa mataifa, lilichukua hatua madhubuti ya kuiadhibu Korea Kaskazini kwa hatua yake ya mwezi uliopita ya kuifanyia majaribio zana zake za kitonoradi.

Katika kura ya pamoja, baraza hilo liliidhinisha vikwazo vipya, vinavyolenga biashara ya chuma na mkaa ya mawe ya Pyongyang ambayo huuza nje bidhaa hizo kwa zaidi ya dola bilioni kwa mwaka.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Korea Kaskazini ikifanyia jaribio kombora

Rais wa Marekani Donald Trump, alipongeza hatua za China na Urusi za kuunga mkono vikwazo hivyo vilivyotolewa na baraza hilo la Umoja wa mataifa.

Anasema kuwa, vikwazo hivyo, vitakuwa na "athari kubwa mno" ya kibiashara.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Katika kura ya pamoja, baraza hilo liliidhinisha vikwazo vipya, vinavyolenga biashara ya chuma na mkaa ya mawe ya Pyongyang

Majirani wao Korea Kusini, wameiomba Korea Kaskazini kufuata njia ya mazungumzo, ili kutanzua mzozo uliopo wa mpango wa Pyongyang, kuhusu zana za kinuklia.

Beijing pia inaomba kurejelewa kwa mazungumzo.