Waliohukumiwa kimakosa nchini China walipwa dola milioni 1.3

Waliohukumiwa kimakosa nchini China walipwa dola milioni 1.3 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waliohukumiwa kimakosa nchini China walipwa dola milioni 1.3

Mahakama ya Uchina imetoa fidia ya dola milioni moja na laki tatu kwa watu wanne, ambao walihukumiwa kifo kwa mauaji katika uhalifu ambao hawakuutekeleza.

Wanaume hao walihukumiwa kifo miaka 14 iliyopita, kwa mauaji na ubakaji wa tajiri aliyekuwa na duka la jumla pamoja na mchumba wake.

Hukumu ya kifo ilipunguzwa na kuwa kifungo cha maisha, na wanaume hao walibaki gerezani kwa zaidi ya miaka 14, hadi mwanamme mwingine alipokiri kuhusika.

Wanasema waliteswa ili kukiri makosa, na baada ya hapo walidai kwamba hawana hatia.

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita zaidi ya hukumu 30 zilizotolewa kimakosa zilibatilishwa nchini China.

Mada zinazohusiana