Aliyefunga kilo 25 za dhahabu kwenye mapaja akamatwa uwanja wa ndege Bangladesh

Gold bars seized by Bangladeshi customs Haki miliki ya picha Bangladesh Customs Intelligence
Image caption Tani 1.5 za dhahabu imekamatwa katika viwanja vya ndege nchini Bangladesh katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita

Mwanamume ambaye alidanganya kuwa kiwete aliyekuwa akitumia kiti cha magurudumu na ambaye alikuwa amefunga dhahabu ya kilo 25 kwenye mapaja yake, amekamatwa kwenye uwanja wa ndege nchini Bangladesh.

Maafisa wa forodha walishuku wakati waligundua kuwa Jamil Akhter, alikuwa amesafiri mara 13 mwaka huu.

Dhahabu hiyo ya gharama ya dola milioni 1.5 ndiyo kubwa zaidi kukamatwa mwaka huu wakati Bangadesh ilibuka kuwa kituo cha kupitisha dhahabu kwenda nchini India.

Kupanda kwa kodi kwa dhahabu nchini India iliyo mnunuzi mkubwa zaidi wa dhahabu duniani kumechangia kuongezeka visa vya uiafarishaji wa dhahabu kwa njia haramu.

Tani 1.5 za dhahabu imekamatwa katika viwanja vya ndege nchini Bangladesh katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Zaidi ya watu 100 wengi raia wa Bangladesh wengi wahamiaji raia wa Bangladesh wanaofanya kazi nchi za Ghuba, wamekamatwa tangu mwaka 2014 kwa kujaribu kusafirisha dhahabu kupitia viwanja vya ndege vya Bangladesh.

Mitamdao ya usafirishaji wa dhahabu huwajumuisha wahudumu wa ndege, wafanyakazi wa viwanja vya ndege na maafisa wa usalama wafisadi.

Mada zinazohusiana