Wauaji wa mjini Valencia waadhibiwe vikali

Venezuela
Image caption Rais wa Venezuela Nicolas Maduro

Rais wa Venezuela , Nicolas Maduro, ametaka adhabu kali kwa watuhumiwa kumi juu ya shambulio dhidi ya jeshi katika mji wa Valencia.

Rais Maduro amesema mmoja miongoni mwa watuhumiwa hao alikuwa na cheo cha Luteni , wengine ni raia ambao aliwaelezea kama wenye nasaba na jeshi.

Watu wengine wawili walifariki dunia katika mauaji hayo ingawa kikundi kingine cha waasi kilichokuwa na silaha walikimbia katika eneo hilo.

Zoezi kali la kuwatafuta waasi hao linaendelea katika mji wa Valencia.

Awali , mkanda wa video ulioachiliwa katika mitandao ya kijamii uliwaonesha watu waliokuwa wamevalia sare wakisema kuwa Walikuwa wakiongezeka dhidi ya kile walichoita udhalimu wa mauaji. Maandamano yameendelea nchini Venezuela kwa miezi kadhaa sasa dhidi ya rais aliyeko madarakani Nicolas Maduro.