Pence akana kujiandaa kuwania urais mwaka 2020

US President Donald Trump and Vice President Mike Pence at the Rose Garden of the White House in Washington Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mike Pence (kulia)

Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence amekana vikali madai ya ripoti kuwa anajianda kuwania urais mwaka 2020.

Gazeti la The New York Times lilisema kampeni za pembeni zimepangwa kufuatia madai kuwa Donald Trump hatawania tena.

Likinukuu vyanzo tofuati ripoti ya gazeti hilo ilisema kuwa bwana Pence anaweza kuwania Urais ikiwa Trump hatawania tena

Bwana Pence amesema ripoti hiyo ni jaribio la kuvuruga uongozi.

Mshauri wa cheo cha juu katika ikulu ya White House Kellyanne Conway pia aliitupilia mbali ripoti hiyo.

"Ni ukweli kuwa makamu wa rais anajiandaa kwa mwaka wa 2020, kuchaguliwa tena kama makamu wa rais, aliliambia shirika la ABC.

Msemaji wa gazeti la New York Times alitetea ripoti hiyo akisema wana imani na taarifa zao na wataiacha ripoti hiyo kuijieleza yenyewe.

Mada zinazohusiana