Korea Kaskazini yakataa mazungumzo na Korea Kusini

South Korean Foreign Minister Kang Kyung-wha talks to an ASEAN foreign minister during the ASEAN-Republic of Korea (ROK) Ministerial Meeting in Philippine International Convention Center in Pasay city, metro Manila, Philippines 6 August 2017. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mawaziri wa Korea Kaskazini na Kusini wafanya mkutano Manila

Korea Kaskazini imetupilia mbali pendekezo kutoka Korea Kaskazini la kutaka wafanye mazungumzo.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Kang Kyung-wha alikuwa ametoa pendekezo hilo kwa mwenzake wa Korea Kaskazini Ri Yong Hi, pembezoni mwa mkutano wa kikanda siku ya Jumapili huko Manila, Ufilipino.

Vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini vilisema kuwa hakutakuwa na mazungumzo kuhusu mpango wake wenye uta wa nuklia wakati inakumbwa na vitisho kutoka Marekani.

Pia ilipinga vikwazo vipya ilivyowekewa na Umoja wa Mataifa siku ya Jumapili

Msukosuko umeshuhudiwa katika rasi ya Korea miezi ya hivi karibuni huku majaribio kadha ya makombora yakifanywa na Korea Kaskazini.

Baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa siku ya Jumapili lilipiga kura kuwekea Korea Kaskazni vikwazo zaidi.

Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini viliripoti kuwa Bi Kang alisalimiana kwa mkono na bwana Ri wakati wa mkutano uliokuwa mfupi ulioandaliwa na nchi za Asean.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri wa Korea Kaskazini Ri Yong Ho (kushoto)

Mada zinazohusiana