Wacheza filamu Chris Pratt na Anna Faris kutengana baada ya miaka 8 ya ndoa

Anna Faris and Chris Pratt arrive at the 72nd Golden Globe Awards in Beverly Hills, 11 January 2015 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Anna Faris and Chris Pratt said that they "cherished" their time together

Wacheza filamu wa Marekani Chris Pratt na Anna Faris wametangaza kuwa watatengana baada ya miaka minane ya ndoa, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyosambazwa kwenye mitandao.

Wawili hao walikutana mwaka 2007 wakirekodi filamu ya mapenzi ya Take me Home Tonight, walisema kuwa jitihada za kuokoa ndoa yao zimefeli.

Tumejaribu sana kwa muda mrefu, tumeghadhabishwa sana, Pratt aliandika kwenye mtandaa wa Facebook siku ya Jumapili.

Pratt, 38, na Faris, 40, walifunga ndoa mwaka 2008 na wana mtoto wa kiume Jack.

"Mtoto wetu ana wazazi wawili wanaompenda sana kwa sababu tunataka kulifanya suala hilo kuwa la siri. taarifa hiyo ilisema .

Taarifa hiyo pia ilisema kuwa wote walifurahia maisha ya kuishi pamoja na na watandelea kushemiana.

Mada zinazohusiana