Korea Kaskazini yaionya Marekani kufuatia vikwazo vya UN

South Korean soldiers stand guard before North Korea's Panmon Hall (rear C) and the military demarcation line separating North and South Korea, at Panmunjom, on 6 August Haki miliki ya picha AFP
Image caption Msukosuko unaendelea wakati Korea Kaskazini inaendelea na majaribio ya makombora

Korea Kaskazini imeapa kulipiza kisasi na kuhakikisha kuwa Marekani imelipia gharama, kwa kubuni vikwazo vya Umoja wa Mataiafa kufuatia na mpango wake wa silaha za nuklia.

Vikwazo hivyo vilivyoungwa mkono kwa kura nyingi na Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi "ni ukiukaji ya uhuru wa nchi," shirika la serikali la habari la Korea Kaskazini KCNA lilisema.

Kwa upande mwingine Korea Kusini inasema kuwa Korea Kaskazini imekataa ombi la kutaka wafanye mazungumzo.

Vikwazo hivyo vililenga kuzuia mauzo ya bidhaa za Korea Kaskazini kwa theluthi moja.

Uamuzi huo wa Halmashauri ya Usalama wa Umoja wa Mataifa ulitokana na majaribio ya kutupa makombora ya mara kwa mara na Korea ya Kaskazini, jambo ambalo limechangia kuongezeka kwa wasi wasi kwenye rasi Korea.

Katika jibu lake kuu la kwanza Jumatatu, Korea ya Kaskazini imesisitiza kuwa itaendelea kuendeleza mpango wake tata wa silaha za nyuklia. Shirikisho la habari la KCNA linasema serikali ya Pyongyang "haiwezi kuweka kizuizi cha kujitetea cha nyuklia kwenye meza ya mazungumzo" wakati inakabiliwa na vitisho kutoka Marekani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Msukosuko unaendelea wakati Korea Kaskazini inaendelea na majaribio ya makombora

Haya yametokea baada ya ripoti kutokea kwamba mawaziri wa kigeni wa Korea Kaskazini na Kusini wamekutana kwa ufupi Jumapili jioni kwenye jukwaa la kikanda katika mji mkuu wa Filipi, Manila.

Vyombo vya habari vya Korea Kusini vilivyoripoti kuwa waziri wake wa nje wa nchi, Kang Kyung-wha, alimsalimu kwa mkomo mwenzake wa Korea Kaskazini, Ri Yong Ho, katika mkutano mfupi katika tukio rasmi la chakula cha jioni uliofanyika na Chama cha Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia (Asean).

Afisa wa Korea Kusini aliiambia BBC kwamba Bwana Ri alisema mazungumzo ya mshirika wake "sio ya kweli".

Waziri wa kigeni wa China, ambaye ni mshiriki wa karibu wa Pyongyang, aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu: "Hisia yangu ni kwamba Kaskazini haikukataa kabisa mapendekezo mazuri yaliyotolewa na Kusini." Wang Yi aliongeza kuwa China pia iliunga mkono mipango ya Kusini.

Mada zinazohusiana