Umri wa Yoweri Museveni: Alibatizwa miaka mitatu baada ya kuzaliwa

Yoweri Museveni Haki miliki ya picha EPA
Image caption Katiba ya Uganda ilirekebishwa mwaka wa 2006, na kumwezesha Museveni kuwania urais kwa mara ya tatu.

Kwa muda mrefu umri wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni umekuwa mjadala mkali.

Serikali ya Uganda imekuwa ikisistiza kwamba alizaliwa mwaka wa 1944, lakini kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana, upinzani ulimshutumu Museveni na kusema kuwa umri wake sio miaka 71 kama anavyodai bali ni miaka 76 na kwa hiyo, ni mzee mno kuwania urais kwani kikomo cha umri kwa urais ni miaka 75.

Sasa ofisi ya rais imechapisha kile inachosema ni hati ya ubatizo inayosema alibatizwa tarehe 3 Agosti 1947 - miaka mitatu baada ya kuzaliwa.

Hiyo inamfanya awe na umri wa miaka 77 wakati wa uchaguzi mkuu ujao wa Uganda wa mwaka wa 2021, na hivyo basi pia mzee sana kuwania urais kwa mara ya sita

Katiba ya Uganda ilirekebishwa mwaka wa 2006, na kumwezesha kuwania urais kwa mara ya tatu.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la Uganda, Museveni alisema awali kwamba hajui tarehe halisi ya kuzaliwa kwake.

"Wazazi wangu hawakujua kusoma na kuandika na hivyo hawakujua tarehe hiyo," inamtaja akisema, katika tawasifu yake ya 'Sowing the Mustard Seed' iliyochapishwa mwaka wa 1997.

Hata hivyo, amesisitizia waandishi wa habari kuwa ana afya nzuri, na wiki iliyopita alisema hajawahi kuwa mgonjwa kwa zaidi ya miongo mitatu:

Mada zinazohusiana