Polisi wanandoa wafutwa kwa kudanganya kukwea mlima Everest

The Rathod couple on Everest
Image caption Dinesh na Tarakeshwari Rathod walisema kuwa walifanikiwa kukwea mlima huo wa mita 8,850 au futi 29,035.

Polisi wawili wamefutwa kazi baada ya uchunguzi kubaini kuwa madai yao kuwa ndio wanandoa wa kwanza kutoka India kukwea mlima Everest hayakuwa ya kweli.

Dinesh na Tarakeshwari Rathod walisema kuwa walifanikiwa kukwea mlima huo wa mita 8,850 au futi 29,035.

Lakini polisi katika jimbo la Maharashtra siku ya Jumaaua walisema kuwa watu walifanyia picha ukarabati kuonyesha kuwa walifanikiwa kuukwea mlima huo tarehe 23 mwezi Mei.

Uchunguzi ulianza kufanywa wakati madai ya wanandoa hao yalitiliwa shaka na wakwea milima wengine.

Haki miliki ya picha Makalu Adventure
Image caption Dinesh na Tarakeshwari Rathod walisema kuwa walifanikiwa kukwea mlima huo wa mita 8,850 au futi 29,035.

Haijulikani ikiwa polisi hao pia watafunguliwa mashtaka.

Mamlaka nchini Nepal nazo zilitangaza marufuku ya miaka 10 kwa wanandoa hao kukwea mlima Everest baada ya kuamua kuwa madai hayo yalikuwa ni ya uwongo.

Bi na bwana Rathon awali aliwaambia waandishi wa habari kuwa picha zao zilikuwa za ukweli.

Lakini mkwea mlima kutoka jimbo la kusini mwa India la Bangalore Satyarup Sidhantha, baadaye aliviambia vyombo vya habari kuwa picha zilizowasilishwa na wanandoa hao zilikuwa ni zake.

Mada zinazohusiana