Polisi amnunulia mwizi nguo alizoshikwa akiiba dukani

Constable Niran Jeyanesan pictured in an interview Haki miliki ya picha CP24
Image caption Alisema kuwa wakati alifika eneo hilo aligundua kuwa mtu huyo alikuwa akiiba nguo ili avae akienda kufanyiwa mahojiano ya kutafuta ajira

Mwizi wa duka huko Toronto ambaye alishikwa akiiba nguo ili aweze kuivaa kwa usaili alipata fusra asiyoitarajia kutoka kwa polisi ambaye aliitwa kuja kumkamata.

Niran Jeyanesan aliambia kituo cha habari cha CP24 kuwa mfanyakazi wa duka la Walmart, aliripoti kuwa mtu huyo wa umri wa miaka 18 alijaribu kuiba shati, tai na soksi.

Alisema kuwa wakati alifika eneo hilo aligundua kuwa mtu huyo alikuwa akiiba nguo ili avae akienda kufanyiwa mahojiano ya kutafuta ajira.

Hapo ndipo aliamua kumuachilia na kumnunulia nguo hizo.

"Kijana huyu amekuwa akikumbwa na wakati mgumu maishani na anajaribu kutatua hilo kwa kuitafutia familia yake riziki kwa kujaribu kupata kazi," bwana Jeyanesan alisema.

Akiongea na BBC mkuu wa Jeyanean, Paul Bois alipongeza kitendo hicho chake.

Mada zinazohusiana