Kura ya kutokuwa na imani dhidi ya Rais Jacob Zuma yapigwa

President Jacob Zuma Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais Jacob Zuma

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anakabiliwa na kura ya kutokuwa na imani naye muda mfupi unakuja.

Spika wa bunge Baleka Mbete alifanya uamuzi wa kura hiyo kufanyika kwa siri baada ya vyama vya upinzani kupeleka kesi katika makakama ya katiba.

Wanaamini kuwa wabunge kutoka chama kinachotawala cha ANC huenda wakapiga kura ya kumng'oa madarakani Zuma ikiwa itapigwa kwa njia ya siri.

Bwana Zuma ashaponea kura mara 7 za kutokuwa na iimani ambapo hakuna hata moja iliyopigwa kwa njia ya siri.

Takriban wabunge 50 kati ya wabunge 249 wa ANC watahitaji kupiga mkuta dhidi ya Rais Zuma ili kura hiyo iweze kupita.

Jaribio hili la hivi punde kumuondoa madarakani Zuma lilikuja baada ya kumfuta kazi waziri wake wa fedha aliyeheshimiwa sana, Pravin Gordhan mwezi Machi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jaribio hili la hivi punde kumuondoa madarakani Zuma lilikuja baada ya kumfuta kazi waziri wake wa fedha aliyeheshimiwa sana, Pravin Gordhan mwezi Machi

Hii pia ni baada ya madai kuwa Rais Zuma alikuwa na uhusiano wa karibu na familia tajiri ya Gupta ambayo inalaumiwa kwa kujaribu kushawishi maamuzi ya kisiasa ikiwemo kufutwa kwake bwana Girdhan.

Maandamano yamekuwa yakifanyika kote nchini Afrika Kusini kabla ya kura hii huku mji wa Johannesbug ukiwa moja ya maeneo yaliyoathirika zaidi.

Polisi wa mjini Johannesburg wako chini ya dhahadhari kubwa.

Bwana Zuma ataacha kuwa kiongozi wa chama cha ANC mwezi Disemba, kabla ya uchaguzi wa mwaka 2019,

Amempendekeza mke wake wa zamani Nkosazana Dlamini-Zuma aweze kumrithi.

Pia wale wanaowania uongozi wa ANC ni Cyril Ramaphosa ambye ni mwanaharaki wa zamani na mmoja wa wanasiasa matajiri zaidi nchini Afrika Kusini,.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maandamano yamekuwa yakifanyika kote nchini Afrika Kusini kabla ya kura hii huku mji wa Johannesbug ukiwa moja ya maeneo yaliyoathirika zaidi