Uhuru Kenyatta: Tuheshimu matokeo

Rais Uhuru Kenyatta amewataka raia kuheshimu matokeo ya uchaguzi
Image caption Rais Uhuru Kenyatta amewataka raia kuheshimu matokeo ya uchaguzi

Raia wanapiga kura katika uchaguzi mkuu nchini Kenya huku kukiwa na hofu kwamba matokeo yanaweza kuzua ghasia za kikabilia.

Rais Uhuru Kenyatta ametaka kuwepo kwa umoja, akisema kuwa atakubali matokeo na kuwataka wapinzani wake kukubali.

Milolongo mirefu imeshuhudiwa mapema alfajiri huku mikanyagano michache ikiripotiwa.

Idhaa moja ya redio nchini humo imetangaza kuwa mtu mmoja amefariki katika ghasia kusini mwa mji wa Kilifi.

Ushindani ni kati ya rais Uhuru Kenyatta dhidi ya mpinzani wake wa muda mrefu Raila Odinga na unaonekana kuwa wa karibu sana.

Bwana Kenyatta ambaye ana umri wa miaka 55 ni mwana wa rais wa kwanza wa taifa hilo anayetetea kiti chake kwa muhula mwengine na wa mwisho.

Wagombea wengine sita pia wanawania wadhfa huo.