Shughuli ya kuhesabu kura yaanza Kenya

Shughuli ya kuhesabu kura imeanza nchini Kenya muda mchache uliopita baada ya raia kujitokeza kwa wingi na kupiga kura
Image caption Shughuli ya kuhesabu kura imeanza nchini Kenya muda mchache uliopita baada ya raia kujitokeza kwa wingi na kupiga kura

Shughuli ya kuhesabu kura imeanza nchini Kenya muda mchache uliopita baada ya raia kujitokeza kwa wingi na kupiga kura.

Baadhi ya vituo vilivyofunguliwa mapema vilikamilisha shughuli ya kupiga kura na sasa vinahesabu kura hizo.

Hatahivyo baadhi ya vituo vilivyofunguliwa kuchelewa vinaendelea kupiga kura huku tume ya IEBC ikisema kuwa vitangozewa muda kuendelea na zoezi hilo.

Mapema alfajiri milolongo mirefu ya kupiga kura ilishuhudiwa katika maeneo nchini humo.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mwendo wa saa kumi na mbili alfajari.

Wengi wa wapiga kura walipiga kambi katika vituo hivyo usiku kucha wakisubiri kutekeleza haki yao ya uchaguzi.

Baadhi ya vituo vilishuhudia mvua kubwa na hivyobasi kuathiri operesheni za shughuli hiyo .