"El Chapo" Guzman awaajiri mawakili wa hadhi kubwa

Joaquin Guzman Loera, known as El Chapo, arrives in New York following his extradition from Mexico. 19 Jan 2017 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Guzman mwenye umri wa miak 60 alitoroka mara mbili gerezani nchini Mexico

Mlanguzi wa madawa ya kulevya raia wa Mexico Joaquin "El Chapo" Guzman, amewaajiri mawakili wenye hadhi kubwa anapokabiliwa na kesi inayohusiana na ulanguzi wa madawa ya kulevya nchini Marekani.

Mawakili hao ni pamoja na Jeffrey Lichtman na Marc Fernich, ambao ni maarufu kwa mafanikio yao kwa kumtetea mwana wa mkuu wa genge la kihalifu mjini New York John Gotti.

Guzman amekana mashtaka hayo kuwa aliongoza genge kubwa zaidi la madawa ya kulevya duniani.

Anakabiliwa na kifungo cha maisha gerezani ikiwa atapatikana na hatia.

Guzman mwenye umri wa miak 60 alitoroka mara mbili gerezani nchini Mexico.

Alisafirishwa hadi nchini Marekani mwezi Januari na anazuiliwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali mjini New York.

Kesi ya Guzman inatarajiwa kuanza mwezi Aprili mwaka ujao anapolaumiwa kwa kuongoza genge la madawa ya kulevya la Sinaloa.

Bwana Lichtman na Fernich walifaniki kumtetea John Gotti Junior katika kesi iliyojulikana kama Dapper Don

Wakati wa kesi iliyodumua miaka mitano, majaji walishindwa kufikia hukumu dhidi ya John Gotti Junior kwa mashtaka ya mauaji na waliachana na kesi hiyo mwaka 2010.

Mada zinazohusiana