Tetemeko kubwa lakumba kusini magharibi mwa China

Residents gather outside buildings in Xian, China, on 8 August 2017 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Tetemeko hilo lilisikika Xian, umbali wa mamia ya kilomita

Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.0 katika vipimo vya richa limesababisha vifo va takriban watu 13 na kuwajeruhi kadha kwenye mkoa ulio kusini mashariki mwa nchi wa Sichuan.

Tetemeko hilo lilikumba eneo lisilo na watu kusini mwa mkoa wa Sichuan.

Baadhi ya ripoti zinasema kuwa huenda idadi ya waliokufa ikaongezea. Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa eneo lililo maarufu kwa watalii.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi na watoa huduma za dharura wakitafuta waathiriwa

Mkoa wa Sichuan unakumbwa na mitetrko mingi. Zaidi ya watu 70,000 waliuawa wakati tetemeko lilikumba eneo hilo mwaka 2008.

Picha zilionyesha majengo ikiwemo hoteli huko Jiuzhaigou, moja ya asilia maarufu.

Mmiliki mmoja wa hoteli alisema kuwa tetemeko hilo lilikuwa na nguvu kuliko lile la mwaka 2008.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Watalii waliondolewa hotelini

Tume ya taifa inayohusika na majanga nchini China ilinukuu shirika la habari la AFP likisema kuwa hadi watu 100 wameuawawa na nyumba 130,000 kuharibiwa.

Baadhi ya ripoti katika vyombo vya habari vya China zilisema kuwa watalii ni kati ya wale waliouwawa na kujeruhiwa.

Rais Xi Jinping alitaka jitihada zote kufanywa na kuokoa watu waliojeruhiwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption waliojeruhiwa wakitibiwa
Image caption China

Mada zinazohusiana