Tetesi za soka Ulaya Jumatano 09.08.2017 na Salim Kikeke

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Philippe Coutinho

Barcelona wanataka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, ifikapo mwisho wa wiki hii. (Mirror)

Liverpool wamekataa kumuuza Coutinho licha ya maafisa wa Barcelona kwenda England kujadili uhamisho huo na wapo tayari kuongeza dau lao la pauni milioni 120. (Star)

Rais wa Real Madrid Florentino Perez amewaambia waandishi wa habari kuwa klabu yake haina mpango wa kumuuza Gareth Bale, 28, kufuatia Manchester United kumnyatia. (Star)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sergio Busquets

Katika mazungumzo ya faragha Florentino Perez amemuambia Jose Mourinho kuwa yuko tayari kumuuza Bale. (Diario Gol)

Meneja wa Chelsea ameitaka klabu yake kupanda dau kumtaka beki wa Tottenham Danny Rose, 27. (Sun)

Chelsea wanataka kumsajili Joao Cancelo kutoka Valencia. (Sky)

Manchester City wamemuulizia kiungo wa Barcelona Sergio Busquets, 29. (Onda Sera)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Virgil van Dijk

Inter Milan wamejiunga katika mbio za kutaka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Leicester City Riyad Mahrez, 26, baada ya dau la pauni milioni 32, la Roma kukataliwa. Leicester wanataka pauni milioni 50. (Mirror)

Paris Saint-Germain wapo tayari kuwazidi kete Manchester City kwa kutoa pauni milioni 80 kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28. (Independent)

Kylian Mbappe, 18, ameamua kuwa anataka kwenda Paris Saint-Germain, huku PSG wakijiandaa kutoa euro milioni 155 kumsajili mchezaji huyo wa Monaco. (Telefoot)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Ahmed Musa

Chelsea na Manchester United wamepewa ishara ya kumfuatilia beki wa kulia wa PSG Serge Aurier, 24, baada ya klabu hiyo kusema mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast anauzwa. (Telegraph)

Southampton wako tayari kumuacha Virgil van Dijk "aozee benchi" kuliko kumuuza. (Express)

Mazungumzo ya Everton na Swansea kuhusu usajili wa Gylfi Sigurdsson yameporomoka. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Leicester City Ahmed Musa, 24, huenda akajiunga na Hull City. (Leicester Mercury)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na wiki yenye tija na mafanikio.