Rais wa Iran awateua wanawake kuwa makamu wa Rais baada ya kukosolewa

Masoumeh Ebtekar Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Bi Ebtekar ameteuliwa kuwa makamu wa rais

Rais wa Iran Hassan Rouhani amewateua wanawake watatu kuwa makamu wa rais kufuatia shutuma za kuwateua wanaume pekee katika baraza lake la mawaziri.

Makamu wa rais 12 nchini Iran husimamia masuala yanayohusiana na Urais.

Kumekuwa na mwanamke mmoja tu katika baraza la mawaziri nchini Iran tangu mapinduzi wa kiislamu yafanyike nchini humo mwaka 1979.

Baraza hilo la mawaziri ambalo ni lazima liidhinishwe na bunge pia linakosa wanachama wa Sunni. Suni huchukua asilimia 10 nchini Iran iliyo na Washia wengi.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Iran haijawai kuwa na wanawake wabunge

Masumeh Ebtekar ameteuliwa makamu wa rais wa masuala ya familia na wanawake, Laya Joeydi ni makamu wa rais wa masuala ya sheria huku Shahindokht Mowlaverdi akiteuliwa makamu wa rais wa haki za raia.

Wabunge wanatarajiwa kupinga baraza lililoteuliwa kwa sababu nafasi muhimu huidhinishwa na kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei.

Bwana Rouhani alimshinda Ebrahim Raisi mwezi Mei baada ya kuahidi kuwa angeboresha uhusiano na nchi za magharibi.

Mada zinazohusiana