Paul Kagame ashinda asilimia 98.78 ya kura

Rais Paul Kagame wa Rwanda Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Paul Kagame wa Rwanda

Rais wa Rwanda Paul Kagame amethibitishwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa wiki iliopita na tume ya uchaguzi nchini humo kulingana na chombo cha habari cha AFP.

AFP imeripoti kwamba tume hiyo ilimuongezea rais Kagame asilimia ya kura alizopata kutoka 98.63, ikiwa ni takwimu zilizotangazwa hapo awali hadi asilimia 98.79.

Alikabiliana na wapinzani wawili , ambapo hakuna hata mmoja wao aliyefanikiwa kupata asilimia moja ya kura

Rais huyo amekuwa madarakani tangu 2000 na amekosolewa kwa unyanyasaji wa haki za kibinaadamu.