Polisi Tanzania wawaua washukiwa 13 Kibiti
Huwezi kusikiliza tena

Polisi Tanzania wawaua washukiwa 13 Kibiti

Polisi nchini Tanzania imethibitisha kuuawa kwa watu kumi na tatu wanaotuhumiwa kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo mauaji ya polisi na viongozi kadhaa wa serikali hubko Kibiti kusini mwa mkoa wa Pwani wa Tanzania.

Katika mahojiano maalumu na mwandishi wa BBC Aboubakar Famau, msemaji wa polisi nchini Tanzania Barnabus Mwakalukwa amesema pamoja na mauaji hayo, polisi pia imeweza kukamata baadhi ya silaha ikiwemo bunduki, risasi, mabomu pamoja na pikipiki mbili.

Mada zinazohusiana