Wakfu wa Bill Gates watenga dola za milioni 350 kwa miradi Tanzania

Magufuli na Bill Gates Haki miliki ya picha Ikulu, Tanzania

Tanzania imezindua awamu ya pili ya mpango wa matumizi ya mifumo ya kielektroniki kwenye uandikishaji na ukusanyaji wa taarifa za afya ikiwemo usambazaji wa dawa na chanjo kwa watoto.

Moja kati ya mifumo miwili iliyopo kwenye awamu hii ya pili ya mpango huu ni ule wa usimamizi wa utoaji chanjo.

Mpango huo unatarajiwa kuwawezesha wataalam wa afya kutunza na kufuatilia taarifa za chanjo za watoto chini ya miaka mitano hivyo kuongeza ufanisi wa utoaji wa chanjo na kupunguza vifo.

Mfumo huu ambao utagharimu dola za kimarekani mlioni 70 tayari umepata ufadhili wa dola milioni 15 toka kwa Wakfu wa Bill and Melinda Gates.

Mwenyekiti wa taasisi hiyo ambaye pia ni billionea namba moja duniani Bill Gates katika ziara yake ya siku tatu nchini Tanzania amekutana na Rais John Pombe Magufuli na kumweleza taaasisi hiyo imetenga dola Kimarekani milioni 350 sawa na billioni 777.084 za Kitanzania kutekeleza miradi mbali mbali katika sekta ya kilimo, afya na mifumo ya kielektroniki ya upatikanaji wa taarifa.

Rais Magufuli amemshukuru Bw. Gates kwa mchango mkubwa unaotolewa na wakfu wake na kuahidi kuwa Serikali yake itahakikisha fedha hizo zinaleta matokeo yaliyokusudiwa.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii