Paul Mwirigi: Mbunge wa umri mdogo zaidi Kenya

Paul Mwirigi: Mbunge wa umri mdogo zaidi Kenya

Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23 ambaye alikuwa mgombea wa kujitegemea katika uchaguzi huu ndiye atakuwa mbunge mpya wa Igembe Kusini, katika kaunti ya Meru mashariki mwa jiji la Nairobi.

John Paul Mwirigi ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu Somo la Ualimu katika Chuo Kikuu cha Mt Kenya alitangazwa mshindi baada ya kupata kura 18,867 na kumshinda mpinzani wake wa karibu Rufus Miriti wa chama cha Jubilee chake Rais Kenyatta, ambaye alikuwa na kura 15,411.

Ameahidi kuwatumikia wakazi wa eneo lake kwa uadilifu.

Amezungumza na mwandishi wa BBC Anthony Irungu.