Wafanyakazi wapewa likizo Iraq kufuatia viwango vya juu vya joto

Iraqi man cuts a block of ice to sell it in Baghdad, Iraq, 6 July 2017 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Biashara ya barafu imenoga mjini Baghdad

Waziri mku wa Iraq Haider al-Abadi ameamrisha wafanyakaziwote wa serikali kuchukua likizo leo Alhamis kutokana na kuwepo viwango vya juu zaidi vya joto.

Watabiri wa hali ya hewa wanatarajia viwango vya joto kwenye mji mkuu Baghdad kufikia nyuzi 50C leo alasiri

Jito jingi pia linatarajiwa miji ya Basra na Mosul.

Joto hilo jingi linaweza kusababisha ukosefu wa nguvu za umeme.

Viwango vya juu vya joto vinashuhudiwa kote eneo hilo na tayari vimeathiri maeneo ya bara Ulaya siku za hivi karibuni.

Wanasayansi wanaonya kuwa hali hiyo inaweza kusababisha vifo vya watu 52,000 barani Ulaya mwaka 2100 ikiwa chocho hakitafanyika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Mada zinazohusiana