Afisi ya rais wa Marekani ikiwa haina samani

Afisi ya Trump ikiwa bila fanicha Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Afisi ya Trump ikiwa bila fanicha

Umewahi kujiuliza afisa ya rais wa Marekani, maarufu kwa Kiingereza kama Oval Office huwa bila viti, meza na vinginevyo?

Hizi hapa ni picha za afisi hiyo katika hali hiyo.

Ikulu ya White House imekuwa ikifanyiwa ukarabati mkubwa, kwa mara ya kwanza katika muda wa miongo sita.

Sehemu ya jumba hilo inayofahamika kama West Wing inafanyiwa ukarabati mkubwa na mabadiliko makubwa.

Trump atakuwa na bahati akirejea kazini wiki ijayo na kupata kiti chake cha kawaida pahali alipokiacha.

Kwa sasa, yupo kwenye likizo ya kikazi katika kilabu chake cha gofu jimbo la New Jersey, likizo ya siku 17.

Lakini amiri jeshi mkuu huyo wa Marekani anapanga kukatiza likizo yake kwa muda Jumatatu na kurejea Washington DC.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Usiwe na wasiwasi: Kitufe cha rangi nyekundu katika chumba cha mikutano cha Roosevelt
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nyaya zinaonekana katika eneo ambalo meza ya Trump kawaida huwa
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wamkumbuka: Huyu ni aliyekuwa msemaji wa ikulu ya White House Sean Spicer
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kreni zinazotumiwa katika shughuli za ukarabati
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mitambo ya kiyoyozi, ambayo iliwekwa miaka 27 iliyopita, inabadilishwa
Haki miliki ya picha Getty Images
Haki miliki ya picha EPA

Mada zinazohusiana