Serikali ya Kenya yaapa kuwakabili waandamanaji wahalifu

kaimu waziri wa usalama nchini Kenya Fred Matiangi
Image caption kaimu waziri wa usalama nchini Kenya Fred Matiangi

Kaimu waziri wa usalama nchini Kenya Fred Matiangi amesema kuwa polisi hawatasita kulinda maisha ya Wakenya na mali yao kufuatia kukamilika kwa uchaguzi uliokumbwa na utata.

Rais Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi na hivyobasi kuhifadhi kiti chake.

Matiangi alikosoa utumiaji mbaya wa mitandao ya kijamii na kusema baadhi ya raia wamekamatwa.

Amesema kuwa kumekuwa na ghasia katika sehemu chache ambazo amelaumu kutekelezwa na wahalifu.

Upinzani unasema kuwa zaidi ya watu 100 wameuawa ikiwemo watoto kumi ijapokuwa haujatoa ushahidi wowote wa madai hayo.

Umesisitiza kuwa hautakwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.