Scaramucci: Kuna watu wanataka kumtoa Trump Mamlakani

Anthony Scaramucci in interview with ABC News
Image caption Anthony Scaramucci alihojiwa mara ya kwanza tangu afutww kazi

Afisa wa mawasiliano wa muda mfupi katika ikulu ya Marekani, Anthony Scaramucci, amesema kuna watu ndani ya serikali, ambao wanataka kumtoa Rais Trump.

Akizungumza na televisheni ya ABC, alisema Bwana Trump analengwa, kwa sababu hakuwamo kati ya viongozi wa siasa nchini humo.

Alipoombwa ataje majina, Bwana Scaramucci alisema, ameshawataja, na rais anahitaji kuleta watu zaidi walio watiifu kwake.

Alipohudumu kwa siku kumi, Bwana Scaramucci alikosoa watu kadha, pamoja na mkuu wa ofisi ya rais wa zamani, Reince Priebus.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Anthony Scaramucci (katikati) alifutwa baada ya kanda ya sauti kufuja akimtukana mshauri Steve Bannon (kushoto) na Reince Priebus