Shambulio latokea Ouagadougou.

Shambulio limetokea Burkina Fasso
Maelezo ya picha,

Shambulio limetokea Burkina Fasso

Watu wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji wenye msimamo mkali wameshambulia mgahawa mmoja katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.

Watu walioshuhudiwa tukio hilo wamenukuliwa wakisema kuwa watu watatu wenye silaha walishambulia wateja waliokuwa wamekaa nje ya Mgahawa huo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AFP, watu wawili wamejeruhiwa, mmoja akiwa ni raia wa kigeni.

Habari zinasema polisi na wanajeshi walipambana na watu hao wenye silaha, huku milio ya risasi ikisikika mara kwa mara.

Ubalozi wa Marekani mjini Ouagadougou umewaonya raia wake kujihadhari na eneo hilo.

Januari mwaka jana kulitokea shambulio kama hilo karibu na mgahawa huo na kusababisha vifo vya watu 30.