Watu 17 washikiliwa Venezuela

Rais wa Venezuela, katika moja ya hotuba zake Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais wa Venezuela, katika moja ya hotuba zake

Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa nchini Venezuela amesema watu 17 wamekamatwa kufuatia shambulio lililofanywa katika kambi ya jeshi wiki iliyopita.

Jenerali Gustavo Gonzalez Lopez amesema watu hao wanaoshikiliwa ni maaskari na raia.

Amesema watu wengine 23 wanatafutwa kwa kile kilichoelezwa kutenda ugaidi.

Miongoni mwa wanaoshikiliwa ama walio katika orodha ya wanaotafutwa ni pamoja na Wafanyabiashara, Viongozi wa vyama vya wafanyakazi na Wanaharakati.

Jenerali Gonzalez amesema pia silaha zimepatikana.

Kiongozi wa washukiwa wa shambulio hilo, kapteni wa zamani wa jeshi Juan Carlos Caguaripano alikamatwa wiki iliyopita.