Zuma: Kulikuwa na njama za kutaka kuniuwa

Rais jacob Zuma wa Afrika kusini amesema kuwa kulikuwa na njama za kutaka kumuua Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais jacob Zuma wa Afrika kusini amesema kuwa kulikuwa na njama za kutaka kumuua

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini wikendi iliopita alizungumzia kuhusu jaribio la kumuua akisema kuwa aliwekewa sumu na karibu afariki kutokana na msimamo wake wa kiuchumi na marekebisho ya umiliki wa ardhi.

Niliwekewa sumu na ningefariki kwa sababu Afrika Kusini ilijiunga na Muungano wa Brics unaounganisha mataifa ya Brazil, Urusi, India, China na jamii ya kibiashara ya Afrika kusini chini ya uongozi wake.

''Walisema nilikuwa nina mpango wa kuharibu nchi'', alisema Zuyma.

Akihutubia mkutano wa wanachama wa ANC huko Phongolo, Kwa Zulu Natal siku ya Jumapili, rais huyo alisema kuwa alilengwa alipotaka kuweka kwa marekebisho makali ya kiuchumi.

Kulingana na ripoti hiyo kulikuwa na majaribio matatu ya kumuuwa.

Katika kanda hiyo hakusema ni nani aliyejaribu kumuua lakini anasema ni mtu wake wa karibu.

Mada zinazohusiana