Raila Odinga kufichua madai ya wizi wa kura Kenya

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga
Image caption Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga aliyeshindwa katika uchaguzi wa urais uliopita ameliambia gazeti la Financial Times nchini Uingereza kwamba atafichua ushahidi siku ya Jumanne kuhusu vile alivyoibiwa kura.

''Tutauonyesha ulimwengu ulivyochezewa'' .

Bwana Odinga ambaye alikuwa akiwania urais kwa mara ya nne pia alibaini kwamba hatowania tena urais na kwamba aliwataka Wakenya kujua kilichofanyika wakati wa uchaguzi huo.

Huwezi kusikiliza tena
Chebukati: Hatujui upinzani ulitoa matokeo yao wapi

''Sio swala la kuwa mbifansi, Sio swala kuhusu Raila Odinga, Sitawania urais tena......tunataka Wakenya kujua kile kilichofanyika, na kile ambacho ulimwengu haujui kinafanyika''.

Bwana Odinga amedai kwamba wadukuzi waliingilia kompyuta za tume ya Uchaguzi na kuweka hesabu ambazo zilimpatia ushindi rais Uhuru Kenyatta.

Madai hayo hatahivyo yamepuuziliwa mbali na tume ya uchaguzi.