Wakuu zaidi wa kampuni wajiuzulu kutoka kwa baraza la kumshauri Trump

Brian Krzanich, CEO of Intel Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkurugenzi mkuu wa Intel Brian Krzanich

Wakurugenzi wawili zaidi wamejiuzulu kutoka kwa baraza la viwanda la Trump kufuatia kisa cha Charlottesville.

Mkurugenzi mkuu wa Intel Brian Krzanich, na yule wa Under Armour Kevin Plank, wamejiuzulu baada ya kujiuzulu kwa mkurugenzi wa Merck, Ken Frazier.

Kufuatia shinikizo kali, Trump alikosoa makundi yanayotetea maslahi ya wazungu siku ya Jumatatu.

Mwanamke mmoja aliuawa siku ya Jumamosi wakati gari lilivurumishwa kwenda kwa umati wa watu waliokuwa wakiandamana kupinga mkutano wa kutetea maslahi ya wazungu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkuu wa Under Armour (wa pili kulia)

Baada ya kuuliwa kwa mwanamke huyo, bwana Trump alikosolewa kwa kushindwa kulikashifu kundi hilo la mrengo wa kulia na badala yake kuamua kulaumu pande zote.

Bwana Plank aliandika ujumbe katika mtandao wa twitter akikashifu ubaguzi wa rangi.

"Tumehusunishwa na kitendo cha Charlottesville. Hakuna nafasi kwa ubaguzi wa rangi au ubaguzi katika ulimwengu wa sasa. Tunachagua amani na umoja."

Saa kumi baadaye bwana Plank aliandika ujumbe mwingine akitangaza kujiuzulu kwake kutoka baraza la ushauri la Trump.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Donald Trump na Ken Frazier

Wakuu wa makampuni kadha wamejiuzulu kutoka kwa baraza la kumshauri Trump ili kupinga sera zake.

Al;iyekuwa mkuu wa kampuni ya Uber, Travis Kalanick, aliondoka katika baraza hilo mwezi Januari kutokana na sera za uhamiaji za Trump.

Mkuu wa Tesla, Elon Musk na mkuu wa Walt Disney, Robert Iger walijiuzulu mwezi Juni baada ya Trump kusema kuwa atajiondoa kutoka na makubaliano ya mabadiliko ya hewa ya Paris.,

Mada zinazohusiana