Mke wa Mugabe, Grace akosa kufika mahakamani Afrika Kusini

Grace Mugabe with her husband Robert attend a rally of his ruling ZANU (PF) in Chinhoyi, Zimbabwe 29/07/2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Grace Mugabe, 52, ni mke wa pili wa Rais Robert Mugabe

Mke wa Rais wa Zimbabwe Bi Grace Mugabe amekosa kufika mahakamani nchini Afrika Kusini kufuatia madai kuwa alimshambulia mwanamke mmoja akiwa Afrika Kusini.

Polisi nchini Afrika Kusini ilisema kuwa hawakuwa wanajua Bi Grace Mugabe alikuwa wapi.

Mwanamke huyo wa miaka 20 amemshutumu Bi Mugabe wa kumpiga kichwani kwa kifaa cha umeme akiwa hotelini.

Alichapisha picha ya jeraha lake. Bi Mugabe hajasema lolote.

Gabriella Engels alimshtumu Bi Mugabe 52, kwa kumpiga baada ya kumpata akiwa na watoto wake wawili wavulana ndani ya chumba kimoja cha hoteli huko Sandton, mtaa mmoja wa kifahari kaskazini mwa mji wa Johannesburg, kwa mujibu wa mwandishi wa BBC.

Haki miliki ya picha GABRIELLA ENGELS
Image caption Sababu ya mwanamke huyo kushambuliwa haijulikani.

Polisi nchini Afrika Kusini walithibitisha kuwa mwanamke huyo alikuwa ameandisha kesi ya kushambuliwa kwa minajili kumsababishia madhara makubwa ya mwili.

Shambulizi hilo linaripotiwa kufanyika Jumapili jioni.

Waziri wa habari nchini Zimbabwe Christopher Mushowe aliambia BBC kuwa hajafahamu madai hayo.

Bi Mugabe alikuwa nchini Afrika Kusini kutibiwa jeraha alilopata kufuatia ajali ya barabarani mwezi uliopita

Mada zinazohusiana