Aliyekuwa naibu kiongozi wa al-Shabaab alikana kundi hilo

Abu Mansur Robow
Image caption Abu Mansur Robow

Abu Mansur Robow, aliyekuwa kaimu kiongozi wa kundi la al-Shabaab amekana uhusiano wowote na kundi hilo.

Bwana Robo ambaye pia anajulikana kama Abu Mansur, alikuwa akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Siku mbili zilizopita alilihama kundi hilo na kujiunga na serikali.

Abu Mansur Robow ni mmoja wa waanzilishi wa al Shabab akiwa na viongozi wengine wenye siasa kali, kufuatia kushindwa kwa kundi la Islamic Courts Union mwaka 2006.

Alipanda ngazi kwa haraka na kuwa msemaji rasmi na naibu kiongozi.

Hata hivyo alitofautiana na kundi hilo lenye uhusiano la al-Qaeda mwaka 2013 na kubaki kuwa mtoro katika maeneo ya vijijini kusini magharibi mwa Somalia hadi kujisalimisha kwake.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Abu Mansur Robow alikuwa msemaji wa al-shabaab

Mada zinazohusiana