Marekani yampongeza Kenyatta kwa kuchaguliwa muhula wa pili

Uhuru Kenyatta ( kulia) na makamu wa rais William Ruto Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uhuru Kenyatta ( kulia) na makamu wa rais William Ruto

Marekani imewapongeza watu wa Kenya kufutia kumalizika kwa uchaguzi mkuu kwa njia ya amani, na pia kumpongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kwa muhula wa pili.

Marekani pia imewapongeza wagombea, maafisa na watu kwa kuendesha uchaguzi uliokuwa wa amani, ikiongeza kuwa inakaribisha taarifa za waangalizi wote kuhusu uchaguzi huo.

"Tunasumbuliwa na ripoti kuwa baadhi ya maandamano yamekuwa yenye ghasia tunatoa wito kwa wakenya wote kukataa ghasia na kutatua mizozo kwa kufuata katiba ya Kenya na sheria

Tunakaribisha wito wa Rais Kenyatta wa kuwepo amani na umoja wa kaitaifa.

Uchaguzi huu wa kihistoria ni hatua kubwa mbele, na tunawashauri wakenya wote kuungana kwa amani na kuendrlea kujenga nchi yao. Mareknia itandelea kushirikiana na Kenya katika kuhakisha kuwepo kwa amani siku za usoni, taarifa hiyo ilisema.