Iran yatwaa mali ya wafanyakazi wa BBC idhaa ya kiajemi

Photograph of court order freezing assets of BBC Persian staff, former staff and contributors
Image caption Iran yatwaa mali ya wafanyakazi wa BBC idhaa ya kiajemi

BBC imetoa wito kwa mamlaka za Iran kufuta amri ambayo itasababisha kutwaliwa kwa mali ya wafanyakazi wake nchini Iran.

BBC inasema kuwa inapinga kulengwa kwa wafanyakazi wa lugha ya kiajemi, wafanyakazi wa zamani na wachangiaji.

Mkurugenzi wa BBC Francesca Unsworth amesema kuwa sheria hiyo ni ya kuwazuia wafanyakazi kuuza au kununua mali, magari na vitu vingine.

Idhaa ya kiajemi ambayo hupeperusha matangazoi yake kwa njia ta runinga, radio na mtandaoni imepigwa marufuku nchini Iran.

Miaka ya hivi karibuni wafanyakazi wa BBC na familia zao wamekumbwa na dhulumwa na kuhangaishwa na mamlaka za Iran.

Idha ya BBC ya kiajemi ilipata amri ya mahakama ambayo imeorodhesha majina ya wafanyakazi 152, wafanyakaza wa zamani na wachangiji ambao mali yao yametwaliwa na mamlaka za nchi hiyo.

BBC haikujulishwa kuhusu amri hiyo na ilifafahamu tu kuhusu kutwaliwa kwa mali hizo wakati jamaa mmoja wa mfanyakazi katika idha ya kiajemi alijaribu kuza mali ayke.

Mamlaka za Iran hazijatoa taarifa yoyote kuhusu amri hiyo ya mahakama.

Mada zinazohusiana