Wanawafalme wa Saudia waliotoweka

Mwanamfalme Turki akiwa katikati Haki miliki ya picha HUGH MILES
Image caption Mwanamfalme Turki akiwa katikati

Katika kipindi cha miaka miwili iliopita, wanawafalme watatu kutoka Saudia waliokuwa wakiishi Ulaya walitoweka.

Wote walikuwa wakiikosoa serikali ya Saudia. Na kuna ushahidi kwamba wote walitekwa na kurudishwa nchini Saudia ambapo hawajasikika hadi leo.

Mapema alfajiri ya tarehe 12 mwezi Juni 2003 mwanamfalme anapelekwa katika qasri pembezoni mwa mji wa Geneva.

Jina lake ni Sultan bin Turki bin Abdulazizi na qasri hilo ni la mjombake marehemu mfalme Fahd.

Ni mwanamfalme anayependwa sana na babake Abdulaziz bin Fahd ambaye amemwalika kiamsha kinywa.

Abdulazizi anamuuliza Sultan kurudi nchini Saudia ambapo anasema kwamba ukosoaji wake wa serikali ya Saudia utatatuliwa.

Sultan anakataa, hatua inayomfanya Abdul Aziz kupiga simu.

Mtu mwengine aliyeko katika chumba chengine ni waziri wa maswala ya kidini wa Saudia, Sheikh Saleh al -Sheikh pia ambaye naye anaonekana akiondoka na baada ya dakika chache watu waliojifunika uso wanaingia.

Wanampiga Sultan na kumfunga kamba na baadaye anadungwa sindano shingoni mwake.

Baada ya kupoteza fahamu anapelekwa katika uwanja wa ndege na kubebwa na ndege ya Medevac ambayo ilikuwa inamsubiri.

Hayo ndio masaibu yaliomkumba Sultan yakielezwa katika mahakama ya Switzerland miaka mingi baadaye.

Miongoni mwa wafanyikazi wa Sultan waliokuwa wakisubiri katika hoteli ya Geneva kwa yeye kurudi kutoka kwa mkutano wake wa kiamsha kimywa alikuwa afisa wake wa mawasiliano Eddie Ferreira.

''Na huku siku ikiendelea kusonga hakuweza kumsikia tena bwana Sultan', anakumbuka.

Hakuweza kukifikia kikosi cha usalama.Hiyo ndio iliokuwa tahadhari ya kwanza.

Tulijaribu kuwasiliana na mwanamfalme huyo ,hatukupata jibu, baadaye mwendo wa saa nane ,wageni wawili wasiotarajiwa waliwasili.

Balozi wa Saudia nchini Swizterland aliwasili na meneja wa hoteli hiyo na kuwataka watu kuondoka katika jumba hilo , alisema Ferreira.

''Mwanamfalme Sultan alikuwa Riyadh na huduma zetu hazikuwa zikitakikana tena na hivyobasi tulihitajika kuondoka''.

Mwanamfalme Sultana alifanya nini ambacho kinaweza kuilazimu familia yake kumkamata kwa nguvu na kumteka ?

Mwaka uliopita alikuwa amewasili Ulaya kwa matibabu na kuanza kuikosoa serikali ya Saudia.

Aliishutumu serikali hiyo kwa kukandamiza haki za binaadamu ,akalalamika kuhusu ufisadi miongoni mwa wanawafalme na maafisa na kutaka mabadiliko kadhaa kufanyika

Haki miliki ya picha iStock
Image caption Mwanamfalme Turki bin Bandar akutana na waziri wa fedha wa Pakistan 2003

Tangu mwaka 1932, wakati mfalme Abdulaziz, anayejulikana kama Ibn Saudia alipoanzisha Saudia taifa hilo limetawaliwa kifalme.

Halikubali upinzani.

Mwanamfalme Turki bin Bandar wakati mmoja alikuwa meja katika kikosi cha polisi wa Saudia akiwa na majukumu ya kusimamia familia ya kifalme .

Lakini mzozo mkali wa kifamilia kuhusu urithi ulimfanya kufungwa jela na alipoachiliwa alitorokea mjini Paris Ufaransa ambapo 2012 alianza kuchapisha kanda za video katika mtandao wa Youtube akitaka mabadiliko nchini Saudia.

Serikali ya Saudia iliingilia kama vile ilivyomfanya Mwanamfalme Sultan kwa kumsihi mwanamfalme Turki kurudi.

Wakati naibu waziri wa maswala ya ndani alipompigia simu ,mwanamfalme huyo alirekodi simu hiyo na kuchapisha katika mtandao.

''Kila mtu anakusubiri urudi, Mungu akubariki'', alisema naibu waziri.

''Munanisubiri nirudi''?,alijibu Turki.

''Vipi kuhusu barua ambazo maafisa wako walinitumia''?

Kwamba wewe mwana wa kahaba, tutakurudisha kwa nguvu kama tulivyomfanya Sultan bin Turki.

Naibu huyo wa waziri alijibu kwa kutoa hakikisho kwamba hakuna atakayekugusa, mimi ni nduguyo.

''Hapana wanatoka kwako'', alisema Turki.''Wizara ya maswala ya ndani iliwatuma''.

Turki aliendelea kuchapisha kanda za video hadi mwezi Julai 2015.

Na baadaye mwaka huo, alitoweka.

Alinipigia simu kila baada ya mwezi mmoja ama miwili alisema rafikiye ambaye ni mwanablogu na mwanaharakati Wael al-Khalaf.

Baadaye alitoweka kwa miezi minne ama mitano.Nilikuwa na wasiwasi.

Nilisikia na afisa mmoja mwandamizi katika ufalme huo kwamba Turki bin Bandar alikuwa nao.

''Kwa hivyo walimchukua'', ''alikuwa ametekwa''.

Baada ya kutafuta habari kuhusu Turki, nilipata habari moja iliokuwa katika gazeti la Morocco ambalo lilisema alikuwa anatarajiwa kurudi Ufaransa baada ya kuitembelea Morocco, alipokamatwa na kufungwa.

Kufuatia ombi la mamlaka ya Morocco alirudishwa nyumbani baada ya mahakama ya Morocco kutoa amri.

''Kwa kweli hatujui kile kilichompata Turki bin Bandar'', lakini kabla ya yeye kutoweka alimpatia rafikiye Wael nakala ya kitabu alichoandika, ambapo aliandika kuhusu utabiri.

''Kwa mpendwa Wael, habari hizi hazifai kupewa mtu mwengine yeyote hadi ntakapotekwa ama hata kuuawa.Najua nitatekwa nyara ama wataniuwa.

Image caption Saud bin Saif al-Nasr

Pia najua wanavyonyanyasa haki zangu na zile za raia wa Saudia.

Wakati kama ule ambao mwanamfalme Turki alitoweka mwanamfalme mwengine wa Saudia, Saud bin Saif al-Nasr- mwanamfalme aliyependa sana Casino nchini Ulaya na hoteli za bei ya juu alipatikana na hatma kama hiyo.

Mwaka 2014 Saud alianza kuchapisha habari mbaya katika Twitter ambazo zilikuwa zikikosoa ufalme wa Saudia.

Alitaka maafisa wa Saudia waliounga mkono kung'atuliwa kwake mamlakani mwaka uliopita kushtakiwa.

Mwaka 2015 mwezi Septemba Saud aliendelea.

Na baada ya mwanamfalme wa Saudia ambaye jina lake halikutajwa kumuandikia barua mbili za kutaka kufanyika mapinduzi ya utawala wa King Salman, Saudia iliunga mkono ikiwa na mwanamfalme wa pekee kufanya hivyo.

Hilo lilionekana kuwa uhaini na liliangamiza hatma yake.

Siku chache baadaye, aliandika ujumbe katika mtandao wa Twitter: Nataka taifa libadilishe maudhui ya ujumbe huu kuwa shinikizo.

Baadaye kaunti yake ya Twitter ilinyamaza.

Mwanamfalme mwengine ambaye alitoa upinzani ni Khalid bin Farhan, aliyetorokea Ujerumani 2013, anaamini kwamba Saud alidanganywa kuhusu kusafiri kutoka Milan kuelekea Rome ili kuzungumzia kuhusu mpango wa kibiashara na kampuni moja ilio na mizizi ya Urusi na Itali iliotaka kufungua matawi yake katika eneo la Gulf.

Ndege ya kibinafsi kutoka kwa kampuni hiyo ilienda kumchukua mwanamfalme Saud.

Lakini haikutua mjini Rome, ilitua mjini Riyadh, Khaled alisema.

Ilibainika kwamba vyombo vya ujasusi nchini Saudia vilipanga njama hiyo, alidai.

Kwa sasa hatma ya mwanamfalme Saud ni kama ile ya Mwanamfalme Turki amabyo ni kuhudumia kifungo jela.

Hatma inayomsubiri ni jela iliopo chini ya ardhi.

Mwanamfalme Sultan aliyekuwa katika mlolongo wa urithi alihudumia kifungo chake kati ya nyumbani na jela.

Lakini afya yake ilikuwa ikidhoofika , kwa hivyo 2010 , Ufalme ulimkubali atafute matibabu mjini Boston Massachussets.

Kile alichokifanya alipokuwa mafichoni Marekani kiliwashtua Wasaudia, aliwasilisha malalamishi katika mahakama ya Uswizi, akimlaumu mwanamfalme Abdulaziz bin Fahd na Sheikh Saleh al Sheikh kwa kuhusika na utekaji wake 2003.

Wakili wake wa Marekani, Clyde Bergstresse alipata rekodi yake ya matibabu kutoka hospitali ya King Faisal mjini Riyadh ambapo Sultan alikuwa amelazwa mnamo tarehe 13 mwezi Juni 2003 ambapo alikuwa amewekwa mpira wa mdomoni kumsaidia kupumua akiwa hana fahamu huku upande wa chini wa kifua chake ukiwa umepooza kutokana na unyanyasaji aliofanyiwa.

Kwa mara ya kwanza afisa mkuu wa ufalme wa Saudia alikuwa akiwasilisha malalamishi ya uhalifu, katika mahakama ya magharibi dhidi ya mwanachama mwengine wa familia.

Lakini Bergstresser anasema kuwa mamlaka ya Uswizi haikuonyesha kuwa na hamu yoyote na kesi hiyo .

Hakuna lolote lililofanywa kuchunguza kitu kilichofanyika katika uwanja wa ndege.

Ni akina nani waliokuwa marubani? Ipi ilikuwa mipango ya ndege hiyo wakati hiyo ilipotoka Saudia ilipotua?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ndege

Utekaji huo ulifanyika katika himaya ya Uswizi na watu wangetaka kujua ulivyofanyika.

Mnamno mwezi Januari 2016, Sultan alikuwa akiishi katika hoteli moja ya kifahari wakati mwanamfalme Saud bin Saif al-Nasr alipotakiwa kuingia ndani ya ndege.

Alikuwa na mpango wa kumtembela babake,ambaye pia alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa Saudia mjini Cairo, wakati balozi wa Saudia alipompatia yeye na ujumbe wake wa watu 18 akiwemo daktari wa kibinafsi, muuguzi na walinzi kutoka Marekani na Ulaya utumizi wa ndege ya kibinafsi.

Licha ya kile kilichotokea 2003, alikubali.

Maafisa wawili waliokuwa katika msafara wake walielezea vile mambo yalivyotokea.

Wote wamekataa majina yao kutajwa.

Tulitembea katika barabara ya mchanga na mbele yetu kulikuwa na ndege kubwa, iliokuwa na maandishi ya Saudia yameandikwa, alisema mmoja wao.

''Haikushtua sana kwa sababu kulikuwa na wafanyikazi wengine ndani ya ndege.Wote walikuwa wanaume'', alisema mwengine.

Ndege hiyo iliondoka huku runinga ndogo zilizomo ndani zikionyesha kwamba ilikuwa inaelekea Cairo.

Lakini saa mbili na nusu baadaye runinga hizo zilizima. Mwanamfalme Sultan alikuwa amelala kitandani mwake na aliamka saa moja kabla ya ndege hiyo kutua.

Aliangilia katika dirisha lake na kuonekana kuwa na wasiwasi, wafanyikazi wake wa zamani walisema.

Walipobaini kwamba walikuwa wanashuka katika uwanja wa ndege wa Cairo, Sultan alianza kugonga mlango wa rubani na kutaka usaidizi.

Mfanyikazi mmoja wa ndege hiyo alimuagiza mwanamfalme huyo na wafanyikazi wake kutulia katika viti vyao.

''Tulitazama katika dirisha tukaona watu kadhaa wakitoka wakiwa wameshikilia bunduki katika vifua vyao na kuizunguka ndege hiyo'', alisema mmoja wa abiria wa ndege hiyo.

Wakati ndege hiyo ilipokua ikishuka.Wanajeshi na wafanyikazi walimbeba Sultan kutoka kwa ndege hiyo. Aliwalilia wafanyikazi wake kupiga simu katika ubalozi wa Marekani.

Mwanamfalme huyo na wauguzi wake walipelekwa katika nyumba moja ya kibinafsi na kuwekwa katika ulinzi mkali.

Katika ndege hiyo wengine walisubiri wakiwa na wasiwasi mkubwa.

Baadaye walipelekwa hadi katika hoteli na kuzuiliwa kwa siku tatu bila ya pasipoti wala simu na baadaye kuruhusiwa kuelekea katika eneo lolote walilotaka.

Kabla ya kuondoka, afisa mmoja wa Saudia ambaye anatambulika kama mmoja wa wahudumu wa ndege hiyo katika ndege aliomba msamaha.

Alituambia kwamba tulikuwa katika eneo baya wakati mbaya.

Na kwamba aliomba msamaha kwa yote yaliotokea, alisema mmoja wao.

Pamoja na mwanamfalme Sultan takriban raia 18 wa kigeni walitekwa nyara na kupekelwa Saudia na kuzuiliwa na jeshi la Saudia.

Hakujakuwa na habari zozote kuhusu mwanamfalme Sultan tangu kisa hicho.

Niliuliza serikali ya Saudia kujibu madai hayo katika filamu hiyo.

Ilikaataa kutoa tamko lolote.

Kwengineko mwanamfalme Khaled ambaye bado yupo mafichoni nchini Ujerumani ana wasiwasi kwamba pia yeye atalazimishwa kurudi mjini Riyadh.

Image caption Mwanamfalme Khaled

Tulikuwa wanachama wanne wa familia moja nchini Saudia.

Tuliikosoa familia na utawala wake Saudia.

''Watatu kati yetu walitekwa nyara ni mimi pekee niliosalia'',alisema.

'Nina hakika, nimehakikishiwa kwa muda mrefu, iwapo watafanya hivyo, wangekuwa wameshafanya hivyo kufikia sasa .Nina tahadhari kubwa lakini kwa gharama ya kuwa huru''.

Mada zinazohusiana