Vifo vyaongezeka Sierra Leone

Maiti zaendelea kuopolewa na kusakwa Haki miliki ya picha EPA
Image caption Maiti zaendelea kuopolewa na kusakwa

Idadi ya waathirika wa maporomoko ya udongo katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown imeongezeka na kufika mia nne.

Mwandishi wa BBC katika wilaya yenye milima ya Regent amesema zaidi ya miili mia moja zaidi imetolewa kutoka kwenye vifusi siku ya Jumanne na maiti zinaendelea kupatikana kutokana na zoezi gumu la uokozi linaloendelea.

Rais wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma, ameomba msaada wa dharura kwa nchi yake ili usaidie nchi hiyo kukabiliana na kile alichokiita uharibifu ya hali ya juu.

Mazishi ya pamoja yamepangwa ili kupunguza msongamano wa maiti katika chumba cha kuhifadhia maiti.