Mtoto wa miezi sita 'aliyepigwa na polisi' Kenya aaga dunia

Babake Pendo {katikati} nje ya hospitali ya Aga Khan mjini Kusumu
Image caption Babake Pendo {katikati} nje ya hospitali ya Aga Khan mjini Kusumu

Mtoto wa miezi sita aliyejeruhiwa na maafisa wa polisi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi yaliozua utata nchini Kenya amefariki, kulingana na familia yake.

Samantha Pendo alikuwa katika hali mahututi tangu siku ya Ijumaa baada ya kupata majeraha ya kichwa wakati polisi walipovamia nyumba yao katika mtaa wa mabanda magharibi mwa mji wa Kisumu.

Babake Joseph Abanja , aliambia gazeti la Daily Nation: Nataka haki kwa mwanangu.hakuwa akiandamana , babake hakuwa akiandamana pia.Mamake hakuwa akiandamana na badala yake walimuua.

''Nilifanya nilivyoambiwa kwenda kupiga kura na kurudi nyumbani''. Walitufuata hapa na kutupiga''.

Image caption Waathiriwa waliopigwa risasi na maafisa wa polisi katika hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu
Image caption Waathiriwa waliopigwa risasi na maafisa wa polisi katika hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu
Image caption Maafisa wa afya waliokuwa na shughuli nyingi kuwatibu baadhi ya raia waliopata majeraha ya risasi mjini Kisumu kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi

Takriban watu 24 waliuawa katika ghasia ambazo zilizuka baada ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti kulingana na shirika moja la haki za kibinaadamu.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga alisema kuwa uchaguzi huo ulifanyiwa udanganyifu ili kumsaidia rais aliyepo madarakani Uhuru kenyatta kushinda.

Hatahivyo wachunguzi wa kimataifa wanasema kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.